Njombe
Zaidi ya wanafunzi 20 pamoja na wakufunzi kutoka Zanzibar wamefika katika halmashauri ya mji wa Njombe na kujifunza mambo mbali mbali yanayohusu halmashauri hiyo ikiwemo kilimo cha Matunda ya Parachichi pamoja na Miti.
Mwenyekiti wa halmashauri Erasto Mpete pamoja na baadhi ya wataalamu wa halmashauri hiyo akiwapokea kwa niaba ya madiwani na Mkurugenzi ametoa shukrani Kwa wageni hao kuona umuhimu wa kutembelea halmashauri hiyo na kujifunza mambo mbali mbali huku akibainisha kuwa kitendo hicho kinaendelea kudumisha muungano.
"Kwa haya ambayo mmeyapata tunaamini yatakuwa na tija na Sasa tumejifunzo kitu kutoka kwenu Kwasababu kila mahala kuna asili yake ukizingatia ninyi wenzetu kule asilimia kubwa ni bahari"Amesema Erasto Mpete
Muombwa Haji Musa ni Mrajisi Mrajisi kutoka Chuo hicho amesema Msafara wao umeambatana na wanafunzi 20 kutoka Chuo cha Mafunzo wanaosoma kozi mbali mbali ikiwemo ya uandishi wa habari pamoja na wakufunzi wao ambao wametembelea halmashauri hiyo na kujifunza kilimo cha Parachichi pamoja na Miti.
Aidha ametoa wito kwa wananchi wa halmashauri ya mji wa Njombe kufika visiwani Zanzibar na kujifunza uchumi wa Blue.
"Kule kwetu eneo letu ni dogo sana,lakini tuna eneo kubwa la bahari zaidi ya kilomita laki mbili hivyo tumeona Sasa imefika wakati wa kuitumia bahari kwa ajili ya kuimarisha uchumi Kwa hiyo nasi pia tumekuja kueneza hilo Kwa kuwa pia tunazalisha vigaranga wengi wa sato"amesema Muombwa Haji Musa
Baraka Mlawa ni afsia kilimo wa halmashauri ya mji wa Njombe ameeleza namna kilimo Cha Parachichi kinavyofanyika mjini Njombe huku akibainisha kuwa uhitaji wa soko la zao la Parachichi ni mkubwa na kwa sasa Njombe kuna wakulima zaidi ya 1531 wenye zaidi ya hekta 1630 huku msimu wa mavuno wa mwaka jana wakifanikiwa kuuza matunda katika soko la nje zaidi ya tani 1976.
Kwa upande wake John Sanga ambaye ni afisa misitu wa halmashauri ya mji wa Njombe amesema mazao ya misitu yamekuwa na msaada mkubwa kwenye uchumi wa halmashauri hiyo ambapo zaidi unatokana na bidhaa za Mbao zinazouzwa sehemu mbali mbali Tanzania bara na visiwani huku pia akibainisha kuwa Miti imekuwa na faida kubwa kutokana na matumizi yake ikiwemo pia kuzalisha karatasi.
Omary Hamidun Mjomba ambaye ni mkuu wa Msafara huo kwa niaba ya msafara ameushukuru uongozi wa halmashauri kwa mapokezi na mafunzo hayo kwa kuwa anaamini wamejufunza mengi juu ya kilimo cha Miti na Parachichi.
0 Comments