Wizara ya maendeleo ya jamii , Jinsia , Wanawake na Makundi Maalumu imezindua mwongozo wa Kitaifa wa uanzishwaji na uendeshaji wa dawati la kutokomeza vitendo vya ukatili katika maeneo ya Umma.
Kwa Mujibu wa ripoti ya mwaka 2021 imebainisha unyanyasaji wa kimwili , ukatili wa kijinsia kwa njia ya ubakaji na ulawiti , unyanyasaji wa kisaikolojia na rushwa ya kingono ni aina za ukatili ambazo wanawake na watoto walikabiliana nazo mwaka huo.
Waziri wa maendeleo ya jamii , Jinsia , Wanawake na Makundi Maalumu Dr. Doroth Gwajima akizindua mwongozo huo Februari 17, 2023 Moshi Mkoani Kilimanjaro katika soko la Mbuyuni amesema tafiti zinaonyesha katika maeneo ya umma kuna watu wanakatiliwa kijinsia wakitoa au wakipatiwa huduma.
Pia mh. Waziri Dr. Doroth Gwajima , amesema mwongozo huo ni wa kila mdau anaetekeleza agenda ya serikali katika kupambana na ukatili na ana matumaini kila mmoja atausoma na kuutekeleza.
Awali Mkurugenzi msaidizi , maendeleo ya jamii , jinsia , wanawake na makundi maalumu Rennie Gondwe amesema maeneo ya umma yakiwemo masoko, stand za mabasi pamoja na machinjio yamekuwa na malalamiko mengi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa Taasisi ya Equality For Growth Jane Magigita, walioshiriki kuandaa mwongozo huo ,amesema anaamini uanzishwaji wa madawati hayo si tu utaongeza usalama kwa wanawake na wanaume lakini pia utaongeza ufanisi na utendaji kazi wa makundi hayo .
0 Comments