F Ndege za kivita za Uholanzi zazizuia ndege za kijeshi za Urusi juu ya anga ya Poland | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ndege za kivita za Uholanzi zazizuia ndege za kijeshi za Urusi juu ya anga ya Poland

 


Ndege mbili za Uholanzi F-35 zimeitambua na "kuisindikiza " ndege ya kijasusi ya Urusi na ndege mbili za kivita ambazo zilivuka hadi anga ya Poland, serikali ya Uholanzi imesema.


Kikosi cha anga cha Royal Dutch Air Force kinatekeleza jukumu la polisi wa anga la Nato nchini Poland.


Hii ni mara ya kwanza uzuizi kama huo umefanywa tangu mzozo wa Ukraine uanze.


Ndege hiyo ilikuwa ikiruka nje ya eneo la Urusi la Kaliningrad kwenye pwani ya Baltic, ambayo iko kati ya maeneo ya Nato ya Poland na Lithuania.


Ndege hizo za Urusi zilitambuliwa kuwa ni ndege mbili za kivita za SU-27 Flanker na ndege ya kijasusi ya IL-20M.


Ndege za F-35 za Uholanzi zilisaidiwa na ndege za Ujerumani za Euro kuzisindikiza ndege za Urusi, ambazo amri ya Nato ya anga ilisema "zinahatarisha watumiaji wengine wa anga kwa kupuuza sheria za kimataifa za usalama wa anga".


Kwa sasa Uholanzi ina ndege nane za F-35 zilizowekwa nchini Poland hadi mwisho wa Machi.


Ndege nne kati yazo zimetumwa kufanya kazi ya "polisi wa anga" nje ya Kituo cha Anga cha Malbork ili kufuatilia anga ya Nato katika Ulaya ya kati na mashariki.


Ndege nynegine nne zinashiriki katika misheni ya mafunzo na washirika, lakini "zinaweza kutumika mara moja" ikiwa zinahitajika.

Post a Comment

0 Comments