Watu watatu wamefariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea katika kiwanja kidogo cha Matambwe Selous ambao ni mtumishi mstaafu wa maliasili na utalii, Rubani Bernard Shayo, kutoka kampuni ya Frankfurt Zoological Society (FZS), Aman Mgogolo na Theonas Nota, wakienda doria.
Ajali hiyo imetokea leo Mei 18, 2023, kufuatia ndege ya shirika la Frankfurt Zoological aina ya Cesna 182 na usajili wa namba 5H-FZS kupata ajali muda mfupi tu baada ya kuruka kutoka kwenye kiwanja kidogo cha Matambwe Selous.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili Dkt Hassan Abbas, imeeleza kuwa, Rubani Shayo pamoja na Mgogolo walifariki hapo hapo, huku Askari Mhifadhi Nota, amefariki wakati ndege iliyokuwa ikimuwahisha hospitali kutua katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam.
Kufuatia ajali hiyo Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa mkoa wa Morogoro Adam Malima vifo hivyo.
0 Comments