Na Ezekiel Mtonyole – Dodoma.
Jeshi la kujenga Taifa JKT limewataka wahitimu wa kidato
cha sita waliohitimu elimu ya Sekondari kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za
Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2023.
Akizungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya JKT
Chamwino Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena
amesema vijana hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika makambi waliyopangiwa
kuanzia June 1 hadi June 11, 2023.
“Sanjari na wito huu JKT limewapangia makambi
watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe
01 june hadi 11 June, 2023” amesema.
Ametaja makambi wanayotakiwa kuripoti kuwa ni JKT Rwamkoma
Mara, JKT Msange Tabora, JKT Ruvu Pwani, JKT Mpwapwa na Makutopora Dodoma, JKT
Mafinga Iringa, JKT Mlale Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba Tanga, JKT Makuyuni
Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila Kigoma.
Makambi mengine ni JKT Itaka Songwe, JKT Luwa na JKT
Milundikwa Rukwa, JKT Nachingwea Lindi, JKT Kibiti Pwani na JKT Oljoro Arusha
na kuongeza kuwa kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti
katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi Pwani ambayo ina miondombinu ya kuwahudumia
watu hao.
Ameongeza kuwa “ Orodha kamili ya majina ya vijana hao
Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo ya makambi yalipo na vifaa wanavyotakiwa
kuripoti navyo inapatikana katika tuvuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana
wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2023 kuungana na vijana wenzao ili
kujengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, kufundishwa stadi za kazi, stadi za
maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa” amesema.
Katika hatua nyingine amesema kwa wahitimu watakaokuwa
wanajiunga na vyuo zoezi la udahili litafanyika katika makambi wanakopata
mafunzo na kutakiwa kuripoti katika makambi wakiwa na nyaraka mbalimbali
zitakazokuwa zinahitajika wakati wa udahili ikiwa ni vyeti vya kitaaluma na
nyaraka mbalimbali.
0 Comments