F Simba wavamia kijiji na kuua Ng'ombe wilayani Wanging'ombe | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Simba wavamia kijiji na kuua Ng'ombe wilayani Wanging'ombe

 





Njombe

Simba wawili wamevamia kijiji cha Kijombe kilichopo wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe na kula mifugo (Ng'ombe) na wengine wakijeruhiwa majira ya saa saba usiku wa kuamkia leo July 22,2023  hali iliyosababisha taharuki kubwa ndani ya kijiji hicho.

Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta ametoa rai kwa wananchi kuwa na tahadhari kwa kuwa maeneo hayo yapo karibu na hifadhi ya Ihefu pamoja Mpanga Kipengere na kutotembea usiku kipindi ambacho wanyama hao wakali wanatafutwa kwa kuwa pia inawezekana maeneo hayo kuwa mapito ya wanyama.

"Tumefika ili tuwape pole kwa kile kilichotokea lakini tunashukuru Simba hao hawajamjeruhi bianadamu,tunatambua tuko karibu na hifadhi ile ya Ihefu lakini pia upande wa Magharibi tuna mpanga Kipengere kwa hiyo inawezekana wanyama hawa wanasafiri kutoka mbuga moja kwenda nyingine kwa hiyo hilo tujue na tuchukue tahadhari wakati huo utulivu uendelee"amesema DC Kitta

Ofisa wanyama pori hifadhi ya Mpanga Kipengere Dominick Rwebangira ametoa rai kwa wakazi wa kijiji kuto tembea tembea kwa kipindi cha siku mbili mpaka tano kwa kuwa askari watakuwa ndani ya kijiji hicho wakiwatafuta wanyama hao huku wakiwa na silaha kali.

Post a Comment

0 Comments