Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemteua Anna Makinda kuwa Mkuu wa Chuo cha Ushirika Moshi.
Taarifa ya uteuzi huo imetolewa leo Agosti 18, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu ambapo pia amemteua Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Aman Abeid Karume kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).
0 Comments