Jeshi la Israel limesema kuwa ndege zake "zimeshambulia kwa mabomu shabaha za kigaidi" za Hezbollah kwenye ardhi ya Lebanon.
Limeongeza kuwa shambulio hili la bomu limewadia kutokana na operesheni zilizofanywa na kundi hilo katika mpaka wa kaskazini wa Israel.
Jeshi lilieleza kuwa operesheni iliyoifanya ni pamoja na kurusha makombora ya vifaru kuelekea kaskazini mwa Israel na kwamba "ilishambulia vyanzo vya urushaji risasi vya kundi hilo huko Lebanon
Limesema katika ujumbe kwenye tovuti ya X kwamba walengwa ni "jengo la kijeshi la Hezbollah, eneo la kijeshi na miundombinu inayotumika kutekeleza operesheni na shughuli ambazo alizitaja kuwa za 'kigaidi' dhidi ya Israel." Hata hivyo, BBC haikuweza kuthibitisha hili.
Katika mkutano na waandishi wa habari, Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema Hezbollah imefyatua "zaidi ya makombora 1,000 kwenye shabaha za Israeli" tangu kuanza kwa vita - lakini "inakabiliwa na uharibifu mkubwa zaidi.
0 Comments