F Ukraine yapigwa na 'Mawimbi' ya mashambulio ya droni za Urusi kwa usiku wa pili mfululizo | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ukraine yapigwa na 'Mawimbi' ya mashambulio ya droni za Urusi kwa usiku wa pili mfululizo


Mkuu wa utawala wa mji wa Kyiv Serhiy Popko, amesema mifumo ya ulinzi wa anga ya Ukraine iligonga takriban droni 10 katika mji mkuu Kyiv na viunga vyake.


Hakuna "uharibifu mkubwa" au majeruhi yaliyoripotiwqa, alisema.


Wakati huo huo, mamlaka ya Urusi ilisema ndege isiyo na rubani ya Ukraine iliyokuwa ikielekea Moscow ilidunguliwa siku ya Jumamosi.


Wizara ya ulinzi imesema ndege hizo zisizo na rubani (UAVs) zilinaswa kwenye Wilaya ya Bogorodsky kwenye viunga vya kaskazini-mashariki mwa mji mkuu.


Meya wa Moscow Sergei Sobyanin alisema hakuna uharibifu au majeruhi.


Mashambulizi ya anga ya Jumapili dhidi ya maeneo yanayolengwa na Ukraine yamefuatia wimbi la mashambulio yaliyotokea usiku wa kuamkia jana, huku Kyiv ikisema kuwa imeangusha ndege 29 kati ya 38 za Shahed zilizotengenezwa na Iran zilizorushwa na Urusi.


BBC haiwezi kuthibitisha ni ngapi ndege zisizo na rubani zilizorushwa na kuharibiwa.


Siku ya Jumamosi, rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alilisifu jeshi lake la anga kwa kudungua UAVs - idadi kubwa zaidi ya mashambulizi ya Urusi iliyoripotiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki sita.

Post a Comment

0 Comments