F Babati mji yatoa tahadhari uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu . | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Babati mji yatoa tahadhari uwepo wa ugonjwa wa Kipindupindu .


Na John Walter-Babati

Mganga mkuu wa Halmashauri ya mji wa Babati Kyabaroti Peter amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwa kufanya usafi na kuzingatia matumizi sahihi ya vyoo, kula vyakula vya moto pamoja na kunywa maji safi na salama ili kuepuka ugonjwa wa Kipindupindu.

Hayo ameyasema leo februari 26, 2024 katika mkutano wa hadhara wa mkuu wa wilaya  na wananchi wa Kata ya Maisaka  mara baada ya kubaini kuwa ugonjwa huo upo katika mji wa Babati.

Amesema ugonjwa huo umezua hofu na kulazimika Halmashauri kusitisha shughuli za mnada wa Gendi uliokuwa ufanyike leo kwa kuhofia ugonjwa huo hatari.

“Niwaombe wananchi kuzingatia usafi, kuepuka kula kwenye mikusanyiko ya watu wengi kama msibani, na kwa mtu ambaye ana dalili za ugonjwa huo ikiwa ni kutapika na kuharisha basi awaishwe kwenye kituo cha afya na mtoe taarifa kwa viongozi ili hatua za haraka zichukuliwe” amesema Dr Kybaroti

Aidha amesema kila mwananchi anawajibu wa kulinda afya yake na familia yake kuwakinga  na mlipuko huu wa kipindupindu kwa kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu.

Mambo muhimu  ya kufanya ili kujihadhari na ugonjwa wa Kipindupindu kama ifuatavyo :-

i. Kunawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula, na mara baada ya kutoka chooni.

ii. Kula vyakula vya moto.

iii. Kuchemsha maji ya kunywa.

iv. Kuosha matunda kwa maji safi na salama.

 v. Kuacha kununua vyakula vya kupikwa kwenye maeneo ya wazi.

vi. Kufanya usafi kwenye maeneo yanayowazunguka.


Post a Comment

0 Comments