Na John Walter -Manyara
Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Dk Shogo Mlozi aliyefariki dunia juni 13,2024 jijini Arusha unazikwa leo juni 17,nyumbani kwao Kijiji cha Endasak wilaya ya Hanang' mkoani Manyara.
Dr. Shogo Richard Mlozi alifariki akiwa njiani kuelekea hospitali chanzo kikitajwa ni kiwango cha chini cha oksijeni katika mfumo wa damu.
Amefariki akiwa na umri wa miaka 45, na ameacha watoto wawili mapacha wenye siku 17 aliofanikiwa kuwapata kwa njia ya upasuaji katika kliniki old Arusha.
Mamia ya watu wakiwemo wabunge na viongozi mbalimbali wamehudhuria mazishi hayo.
Dr. Shogo alichaguliwa kuwa Mbunge wa Afrika Mashariki mwaka 2022 ambapo angehudumu hadi mwaka 2027.
Dr. Shogo ni mke wa mkuu wa chuo cha Uhasibu Arusha-IAA Profesa Eliamani Sedoyeka.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
0 Comments