Mstahiki Meya wa halmashauri ya jiji la Dar es salaam Mhe. Omary Kumbilamoto jana Juni 5, 2024 amekabidhi msaada wa mabomba ya kusambazia maji kwenye mtaa wa Misewe kata ya Liwiti baada ya wananchi kukosa huduma maji kwa siku tano kutokana na matengenezo ya barabara ya mtaa huo yaliyopelekea kukatika kwa mabomba.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo Meya Kumbilamoto alisema alipokea kero hiyo kutoka kwa Diwani wa Kata ya Liwiti, Alice Mwangomo baada ya greda ambalo lilikuwa linakarabati barabara kukata mabomba hivyo kumlazimu kutafuta wadau wa maendeleo ili kunusuru adha ya maji kwa wananchi wanaoishi eneo hilo.
''Nichukue nafasi hii kuwapa pole wananchi wote mliokosa hudama ya maji, na hiki nilichokifanya leo ni maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia ambaye ametuelekeza wasaidizi wake kutatua kero za wananchi hivyo nimeleta mabomba haya yenye thamani ya shilingi milioni 1.5 ambayo yatatumika kurudisha miundombinu ya maji kama ilivyokuwa awali'' alisema Meya Kumbilamoto
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE
0 Comments