FCC yatakiwa kushirikiana na Taasisi, wadau kusaidia kupunguza athari ya matumizi ya bidhaa bandia


Serikali imeiagiza Tume ya Ushindani (FCC) kuhakikisha inashirikiana na Taasisi, wadau mbalimbali ili kusaidia kupunguza athari kubwa ya matumizi ya bidhaa bandia ambazo sio sahihi kwa ukuaji wa uchumi jambo ambalo litapeleka kukosa mapato, kupoteza ajira kwa vijana na kukosa fursa mbalimbali za uwekezaji.

Agizo hilo limetolewa leo Julai 18,2024 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb) kwaniaba Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb) wakati akimuakilisha kwenye kilele cha Maadhimisho ya Kitaifa ya siku ya kudhibiti bidhaa bandia Duniani.

Mhe. Kigahe amebainisha kuwa ili kupambana na kudhibiti matumizi ya bidhaa bandia nchini kuna umuhimu mkubwa wa kushirikiana kwa pamoja ili kudhibiti bidhaa hizo katika kuvutia wawekezaji kuwekeza wakiamini Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji na kufanya biashara.


Aidha, Dkt. Godwin Osoro Mjumbe wa Tume ya Ushindani (FCC) akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Bodi amesema wanaendelea na mchakato wa kudabilisha sheria ya udhibiti bidhaa bandia ili kuendana na mazingira ya sasa kutokana mabadiliko ya sayansi na teknolojia huku wa kiwaasa wafanyabiashara na wadau wengine kuendelea kuwaunga Tume kwa kutoa elimu kwa wateja ili waweze kutambua bidhaa hizo na waweze kununua bidhaa halisi.

Naye Jaji Butamo Kasuka Philip akizungumza kwa niaba ya jaji kiongozi amesema ni jukumu la pamoja kushirikiana katika kulinda wananchi katika kuepukana na bidhaa bandia ili kuhakikisha wanapata bidhaa halisi


Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani FCC William Erio alisema kuwa licha ya elimu kutolewa kwa wananchi juu ya utambuzi wa bidhaa bandia bado kuna haja ya kuendelea kuzungumza na wafanyabiashara umuhimu wa kuweka alama au nembo katika bidhaa zao huku Ummy Mohamed Rajab kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa ZFCC amesema athari za matumizi ya bidhaa bandia hazilengi kudumaza uchumi wa nchi pekee bali hata kwa watumiaji.

Pia alizitaja shughuli mbalimbali zilizofanyika tangu kuanza kwa maadhimisho hayo hadi kilele chake ambazo ni pamoja na utoaji elimu wa kuacha matumizi ya bidhaa bandia kupitia vyombo vya habari, kufanya moanesho ya wamiliki bidhaa katika ukumbi wa mlimani city Jijini Dar es salaam.



Post a Comment

0 Comments