Kila kijiji kusambaziwa Umeme kwa Kilomita mbili.



Na John Walter -Babati 

Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Daniel Sillo amewaondoa wasiwasi wananchi ambao maeneo yao hayajafikiwa na umeme kwamba tayari nguzo zishaanza kusambazwa kwenye maeneo yao.

Amesema nguzo 40 kila kijiji zitasambazwa kusambaza umeme kwenye vijiji kwa kilomita mbili na baada ya hapo itafuata kwenye vitongojim lol

Amesema serikali inamkataba na Wananchi wake kupitia ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi mwaka 2020-2025 ambayo inaendelea kutekelezwa vyema kupitia miradi mbalimbali ya Maendeleo.

Sillo ameyazungumza hayo akiwa kwenye mkutano wa hadhara kijiji cha Bashnet wilaya ya Babati mkoani Manyara kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi.

Sillo amesema kwa kushirikiana na Chama cha Mapinduzi na Serikali watahakikisha huduma zote muhimu zinafika katika maeneo ambayo hayajafikiwa kwa ajili ya Maendeleo ya Wananchi.

Kwa mujibu wa Afisa mahusiano wa TANESCO mkoani Manyara Kelvin Kasambala, baada ya umeme kufika kwenye vijiji,katika mwaka huu mpya wa fedha umeme unaingia ngazi ya vitongoji.

Ameongeza kuwa TANESCO haipokei fedha mkononi bali kwa njia ya malipo kupitia namba maalum (control number) hivyo Wananchi waepuke matapeli.

Post a Comment

0 Comments