Mati super brand's Ltd ndo mdhamini wa Fountain Gate Fc

Na John Walter -Babati 

Kampuni ya Mati Super Brands Limited inayozalisha vinywaji changamshi iliyopo mjini Babati Mkoani Manyara  imedhamini timu ya mpira wa miguu  inayoshiriki ligi kuu ya soka Tanzania bara ya Fountain Gate fc kupitia kinywaji chake kipya  cha Tanzanite Royal Gin ambapo timu hiyo imeingia makubaliano ya udhamini wa mwaka mmoja na kampuni hiyo .

Akizungumza katika Hafla ya kusaini mkataba wa udhamini huo,Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited David Mulokozi amesema kuwa wameamua kudhamini timu hiyo ili kutoa fursa kwa wakazi wa Mkoa wa Manyara kupata burudani ya soka kutoka kwa timu ya Fountain Gate fc na kunufaika na  fursa za uwepo wa timu hiyo na timu mbalimbali zitakazofika mkoani hapa ikiwemo wafanyabiashara,wajasiriamali .

Mulokozi amesema kuwa uwepo wa timu hiyo utachochea maendeleo ya michezo mkoani Manyara Pamoja na maendeleo ya kiuchumi kutokana na timu hiyo kupiga kambi mkoani Manyara .

“Leo Tumewaletea Habari Njema kwa mkoa wa Manyara kuwa timu hii pendwa ya Fountain Gate imehamia Mkoani Manyara chini ya Udhamini wa Kampuni ya Mati Super Brands Limite kupitia kinywaji kipya cha Tanzanite Royal Gin” Anaeleza David Mulokozi Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited.

Mkurugenzi wa Timu ya Fountain Gate Japhet Makau ameishukuru Kampuni ya Mati Super Brands Limited kwa udhamini mnono na kuahidi kufanya vizuri katika mashindano mbali mbali ya kitaifa na kimataifa.

Afisa Mtendaji Mkuu  Timu ya Fountain gate kidawawa Thabita amesema wachezaji wote wana hali nzuri na wako tayari kushiriki mashindano wakati wowote na kuongeza kuwa udhamini huo utaongeza ufanisi mkubwa kwenye timu hiyo.

Post a Comment

0 Comments