Mbunge Rahhi awapa Vijana na Wanawake mbinu za kujiajiri.

Na John Walter-Babati 

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara Mheshimiwa Yustina Rahhi ameendelea kuwawezesha Vijana na Wanawake mkoani humo kwa kugharamia Mafunzo yatakayowawezesha kuweza kujiajiri na kuacha kutegemea  ajira kutoka serikalini.

Mpaka sasa Mheshimiwa Rahhi ameshawawezesha Vijana na Wanawake wa wilaya za Mbulu, Kiteto, Simanjiro, Hanang'  na sasa wilaya ya Babati.

Mafunzo haya yanatolewa ili kuwajengea uwezo vijana na Wanawake, kuwapa maarifa na kujiajiri katika ujasiriamali.

Akifungua Mafunzo hayo Kata ya Magugu wilayani Babati, Mheshimiwa Yustina Rahhi aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuwakwamua vijana kiuchumi kwa kuwapa maarifa wezeshi yanayowawezesha kupambana na umaskini kupitia shughuli za ujasiriamali kwa kuwapatia mikopo isiyokuwa na riba ili wajikwamue kiuchumi.

Mh. Rahhi amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  anapambana kuhakikisha Watanzania wanaingia kwenye uchumi wa kati ili Kiwango cha pato la mtanzania kifike angalau dola 10 kwa siku.


Amesema bidhaa ndogo ndogo kama karanga na  keki zinatumika kila siku hivyo wajasiriamali waliopatiwa Mafunzo hayo wazalishe kwa wingi bidhaa hizo.

Mh.Rahhi amewataka vijana hao kuyatumia maarifa waliyoyapata kwa weledi na kwa faida yao na jamii kwa ujumla ili kufikia azima ya serikali na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Ujumla.

Post a Comment

0 Comments