F Mji mdogo wa Mirerani kujengwa kwa lami. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mji mdogo wa Mirerani kujengwa kwa lami.

Na John Walter -Simanjiro 

Mwenge wa uhuru mwaka 2024 umeridhia kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa barabara ya sokoni Mirerani -mgodini Tanzanite kwa kiwango cha lami nyepesi urefu wa kilomita 1.2.

Mradi huo utakaotumia  gharama ya shilingi milioni 949.73 kutoka serikali kuu ulianza April 4,2023 na unatarajiwa kukamilika Julai 30,2024.

Kwa mujibu wa taarifa ya mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Lulandala kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa 2024 Godfrey Mnzava, barabara hiyo itasaidia kuondoa kero ya vumbi ambalo ni chanzo cha magonjwa kama kifua kikuu kwa wananchi.

Akiweka jiwe la msingi la Ujenzi wa barabara hiyo, amezitaka taasisi za serikali kuwa wa wazi wakati wa kutafuta wazabuni kupitia mfumo wa kisasa unaojulikana kama NeST.

KAULIMBIU; Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

Post a Comment

0 Comments