Mwenge waweka jiwe la msingi kituo cha Afya Tanzanite


Na John Walter-Simanjiro

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa mwaka 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi ujenzi wa kituo cha Afya Tanzanite katika kata ya Mirerani utakaogharimu Shilingi milioni 500 hadi kukamilika.

Taarifa ya mkuu wa wilaya ya Simanjiro Mwalimu Fakii Lulandala kwa Kiongozi wa mbio za Mwenge, imeeleza kuwa kituo hicho kitakuwa na jengo la wagonjwa wa nje, maabara, jengo pacha la wazazi na upasuaji.

Ujenzi wa kituo cha Afya Tanzanite ulianza machi 22,2024 na kinatarajiwa kukamilika kabla ya mwezi oktoba 2024 ili kutimiza azma ya Serikali kupunguza msongamano wa wagonjwa katika kituo cha Afya Mirerani na kuzidi kusogeza huduma bora za afya kwa Wananchi wa mji mdogo wa Mirerani.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Mnzava baada ya kukagua hatua za ujenzi ameridhishwa na kuweka jiwe la msingi pamoja na kupanda miti katika eneo la Kituo cha Afya huku akisisitiza hatua zillizosalia zikamilishwe kwa wakati na ubora.

Mwenge wa uhuru mwaka 2024 unaongozwa na kaulimbiu isemayo Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.


Post a Comment

0 Comments