F Mwenge waweka jiwe la msingi ujenzi barabara ya lami Mbulu mjini. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Mwenge waweka jiwe la msingi ujenzi barabara ya lami Mbulu mjini.




Na John Walter -Mbulu

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Godfrey Mnzava ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara ya lami  Mbulu mjini na utakaogharimu Shilingi Milioni 474,540,000.

Meneja wa Wakala wa barabara za mijini na vijijini Mhandisi Nuru Hondo amesema ujenzi wa barabara hiyo ni hitaji la muda mrefu la Wananchi ili kutatua kero ya kukatika mawasiliano hasa kipindi cha mvua ambapo barabara jujaa maji na kukwamisha shughuli za kiuchumi na kijamii.

Amesema Mradi huo ulianza kutekelezwa Tarehe 13/9/2023 na unategemewa kukamilika Tarehe 13/8/2024.

 Kaulimbiu ya Mwenge wa uhuru mwaka 2024, Tunza Mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa Ujenzi wa taifa endelevu.

Post a Comment

0 Comments