F RC Sendiga na Sillo waanza mchakato wa kujenga Zahanati Endadosh. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

RC Sendiga na Sillo waanza mchakato wa kujenga Zahanati Endadosh.



Na John Walter -Babati 

Wananchi wa Kijiji cha Endadosh kata ya Qash wilayani Babati wameiomba serikali kuwatazama kwa jicho la huruma na kuwajengea zahanati yenye uwezo wa kutoa huduma za afya kwani kwa sasa hulamizimika kutembea umbali wa kilomita 20 kufuata huduma Galapo.
Wananchi hao wamesema wajawazito hujifungulia njiani na kwamba mwaka Jana walimpoteza mama mmoja  huku akiacha kichanga.

Wametoa kilio chao mbele ya mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga, Mbunge wao Daniel Sillo na Viongozi wa chama cha Mapinduzi wakati wa sherehe iliyoandaliwa na wanakijiji hao kuishukuru serikali kwa kuwapatia huduma ya maji safi na salama, hafla iliyofanyika shule ya Msingi Maleshi.



Hata hivyo kilio chao kilipokelewa na Viongozi hao ambapo mkuu wa mkoa aliahidi mifuko 100, Mbunge Daniel Sillo mifuko 50 ya Saruji huku akifanya chagizo dogo lililowezesha kupatikana mifuko 540 ya Saruji, mabati bando 10 na Mawe roli 10 za mawe.

Mbunge wa Jimbo la Babati vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo amewahakikishia Wananchi kuwa zahanati hiyo itajengwa.

Hata hivyo uongozi wa Kijiji umeeleza kuwa wanalo eneo lenye ukubwa wa hekari 200 kwa ajili ya Ujenzi wa zahanati hiyo.

Post a Comment

0 Comments