SUA kuleta wataalam wa kilimo kutoka China kuwawezesha Watanzania kupata ujuzi wa kilimo


Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   kinatarajia kuanzisha kituo wezeshi cha kuwawezesha wataalamu mbalimbali wa kilimo kutoka china kuja kutoa teknolojia mbalimbali za kilimo, mifugo na uvuvi hapa nchini zitakazowawezesha watanzania kuongeza uzalishaji na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya siku moja  wanafunzi  kutoka chuo kikuu kilimo china,  kutembelea maeneo mbalimbali ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   kwa lengo la kujifunza,  mkurugenzi katika kurugenzi ya udhamiri utafiti ufaulishaji wa teknolojia na ushauri wa kitaalamu  Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   prof; JAPHET kashaigili    amesema  lengo la ziara hiyo ni kushirikiana kwenye utaalamu wa kilimo kutoka nchini China.

Aidha Kashaigili amesema kuwa kupitia mahusiano haya wanatarajia kupata teknelojia itakayomwezesha mkulima kulima kilimo chenye tija pia yatawezesha kujenga kituo wezeshi cha kilimo ndani ya Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   kwa ajili ya kuendesha makongamano kwa wataalam kutoka china, kuja kuonyesha utaalamu mbalimbali kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla.

“kituo hiki kitawazesha vijana kupata utaalamu wa kutosha kuhusu kilimo, na mahusiano haya tuliyaanza yaweze kuwa na tija na yawe endelevu na paia kitakuwa na maabara mbalimbali  za uzalishaji na teknologia zitakuwepo za kutoka china tena wezeshi pia zitakuwa za kibiashara ambapo china na Tanzania zitapata faida kupitia kituo hiicho, leo hii tumepokea wanafunzi kutoka china na walimu wao kwa lengo la kubadilishana mawazo na kujifunza na sisi tulivyokwenda kwao. alisema prf; Kashaigili”.

Kwa upande wake  Profesa Xu Xiuli  kutoka chuo kikuu cha kilimo china amesema lengo la ziara yao kuja Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA)   ni kutembelea na kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo na kubadilishana uzoefu.

Post a Comment

0 Comments