Na John Walter -Babati
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Babati Mheshimiwa Lazaro Twange leo septemba 5,2024 amemkabidhi rasmi ofisi mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na wakuu wa taasisi za serikali, wenyeviti wa Halmashauri, wakurugenzi pamoja na taasisi za kifedha zilizopo Babati.
Mhe. Twange amehamishiwa wilaya ya Hai Mkoani Kilimanjaro huku Emmanuela akihamishwa kutoka Arumeru mkoani Arusha.
Tayari Twange amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Amir Mkalipa aliyehamishiwa wilaya ya Arumeru.
Viongozi hao wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwaamini kumsaidia kutumikia Wananchi.
Mh. Emmanuela Kaganda ameahidi ushirikiano kwa Wananchi na idara zote za serikali na binafsi kama alivyokuwa akifanya mtangulizi wake Lazaro Twange.
0 Comments