FCC yaahidi kuendelea kutekeleza utendaji unaozingatia sheria


TUME ya Ushindani (FCC), imeahidi kuendelea kutekeleza na kulinda majukumu yake ya ushindani nchini kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya serikali ili kufanikisha malengo yaliyokusudiwa ya kutoa huduma iliyo bora kwa wananchi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa FCC, William Erio leo Septemba 23, 2024 alipokuwa akitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Ofisi ya kumbukumbu na Nyaraka za Taifa, Firimin Msiangi mra baada ya semina ya mafunzo iliyofanyika katika ofisi za Ushindani, jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Urio ameeleza kuwa, FCC watahakikisha wanatekeleza yote waliyoagizwa na ofisi ya kumbukumbu kuhakikisha kuwa yanatekelezwa na watayafanyia kazi.

"Tunakushukuru kwa semina hii nzuri inayotoa miongozo mbalimbali ya serikali inayotakiwa kutekelezwa katika Taasisi mbalimbali za Umma na uzingatiaji wa nyaraka za serikali na walaka wa mwaka 2000 wa kuzingatia taarifa sahihi na salama za serikali," amesema

Ameongeza kuwa kila mtumishi wa taasisi hiyo atasimamia majukumu yake na kutekeleza wajibu kwa umma ili kufikia malengo ya serikali bila kuathiri usiri au unyeti wa nyaraka za serikali.

"Maagizo uliyoyatoa yanalenga sana kwetu sisi viongozi wa umma, pia, yanagusa watumishi wa taasisi ambao tunashirikiana nao katika kutekeleza majukumu ya serikali, hivyo tutahakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake," amesema.

Aidha Mkurugenzi Urio, amemshukuru Mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa ya kutoa semina na mafunzo hayo yenye tija kubwa katika utumishi wao kwa jamii.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ofisi ya Kumbukumbu na uhifadhi nyaraka za serikali, Firimin Msiangi amepongeza FCC, kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kutimiza majukumu ya serikali hukuakiahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuwajengea uwezo wa kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia.


 




Post a Comment

0 Comments