F KUFUNGWA KWA DIRISHA LA MASAHIHISHO MAOMBI YA MIKOPO 2024/2025 ZIMEBAKI SIKU TATU | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

KUFUNGWA KWA DIRISHA LA MASAHIHISHO MAOMBI YA MIKOPO 2024/2025 ZIMEBAKI SIKU TATU


Bodi ya Mikopo Tanzania (Heslb) inapenda kutoa taarifa kwa Waombaji wa Mikopo ya Wanafunzi kwa Mwaka 2024/2025 kuwa baada ya kufanya uhakiki wa maombi yao, imebainiwa baadhi ya maombi hayo yanahitaji kufanyiwa masahihisho ili kuruhusu kuendelea kwa hatua inayofuata.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo Dkt. Bill Kiwia amesema ‘Tunapenda kuwataarifu waombaji wote wa Mikopo ya Elimu ya Juu kuwa tunatarajia kufunga dirisha la Masahihisho ya maombi ya Mikopo ifikapo tarehe 21.09.2024 saa 5:59 Usiku.Wote walioomba Mikopo wanashauriwa kuingia kwenye akaunti zao walizotumia kuomba mikopo kuona iwapo wanahitajika kufanya marekebisho’

Aidha, Maombi mapya hayatapokelewa kwani dirisha la maombi ya mkopo kwani limefungwa rasmi Septemba 14, 2024.

Post a Comment

0 Comments