Mati super brands yapewa tuzo ya heshima na JWTZ


Na John Walter -Babati 

Kampuni ya vinywaji burudishi ya Mati Super Brands Limited imepewa tuzo maalumu kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania kwa kutambua mchango wao katika kusaidia jamii inayowazunguka pamoja na kushirikiana na Serikali.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati super brand's Ltd David Mulokozi na  Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC), Colonel Verus Chrysostom Mbuzi walipofika kiwandani hapo mjini Babati katika ziara maalumu ya kimafunzo iliyofanywa na Maafisa wa ngazi za juu wa Kijeshi kutoka mataifa mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited, David Mulokozi amesema kuwa Tuzo hiyo inawapa heshima na nguvu ya kuendelea kufanya vizuri huku wakiendelea kushirikiana na taasisi za umma pamoja na kuzalisha bidhaa bora zinazozingatia ubora na usalama kwa mtumiaji.

Post a Comment

0 Comments