F Naibu Waziri Daniel Sillo aendesha Harambee Ujenzi wa Kanisa la AGAPE | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Naibu Waziri Daniel Sillo aendesha Harambee Ujenzi wa Kanisa la AGAPE

Na John Walter -Babati 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Babati Vijijini Mheshimiwa Daniel Sillo, ameendesha harambee na kuchangisha shilingi milioni 1,912,000 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Agape lililopo Kijiji cha Hoshan kata ya Duru, Wilaya ya Babati, mkoani Manyara.

Katika hafla hiyo, Sillo aliwasihi wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao, akisisitiza umuhimu wa kuwafundisha maneno ya Mungu ili wawe raia wema katika jamii. Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeweka mazingira mazuri kwa watu wote kuabudu kwa amani na utulivu katika nyumba za ibada 

Kwa upande wake Mchungaji wa Kanisa la Agape Sanctuary Churches International Tanzania alimshukuru Naibu Waziri Sillo kwa kuweza kufika na kusaidia harambee hiyo pia katika risala yake, alieleza kuwa kanisa hilo lilianzishwa mwishoni mwa mwaka 2018 na sasa lina waumini zaidi ya 40.

Aidha aliongeza kuwa ujenzi wa kanisa hilo upo katika hatua ya lenta, ambapo kwa sasa wanahitaji mabati, mbao, milango, na madirisha ili wakamilishe ujenzi huo wa Kanisa

Post a Comment

0 Comments