Na MWANDIDHI WETU
Kinachoendelea nchini kwa wiki kadhaa saaa ni baada ya baadhi ya watu kudaiwa kutekwa , kutoonekana mahali waliko huku mtu mjumbe wa sekreteriet ya CHADEMA kukutwa amauawa .
Watu kutekwa,kuteswa,kujeruhiwa si kitu ambacho kimo katika nasabu za utamaduni wa Taifa la Tanzania.
Hata hivyo jambo hili linahitaji watu wazima makini kukubaliana na kukaa chini; kutafakari na kufikia jinsi gani yatakavyokomeshwa yasiendelelee kutokea.
Kwa kifupi watanzania wote kwa miaka yote sitini ya kujitawala wenywee , tumekuwa katika kazi ya kujenga nyumba moja hivyo (Taifa)hakuna haja , sababu wala mantiki ya kugombania fito
Kitendo cha kuendelea kutuhumiana kila uchao labda jambo hili linaendeshwa na upande wa utawala au upinzani hizo ni hisia batili na fikira chakavu zilizokosa mashiko ya kutosha.
Tatizo linapozuka na kuwa la kitaifa ,viongozi katu hawapaswi kubabaika na kutaharuki, badala yake lazima wote wakae pamoja kama taifa ili kupatia utatuzi wake kwa kuhakikisha waharifu wanapatikama katika kulinda usalama wa Taifa.
Ikiwa utawala utautuhumu upinzani kuhusika na matukio hayo au upinzani kushiklia matendo hayo yanafanywa na vyombo vya dola,pia hizo ni fikra mfu zisizo na maana kamili.
Majibu ya maswali yote hayo hayatapatikana kwa kunyooshena vidole ,badala yake huko ni kupoteza wakati ,kufuja muda wa kuzalishamali na kukwamisha dhana ya maendeleo bila kupata tiba ya kadhia hiyo nchini.
Katika siku za hivi karibuni kupitia kongamano la ekaristi ya tano, liloifanyika katika uwanja wa uhuru jijini dar es salaam , kumetokea tukio au jambo linalohitaji kina cha mazingatio kulizingatia.
Viongozi kadhaa wa kisiasa nao wamwshiriki kwenye kongamano hilo akiwemo Makamo Mwenyekiti wa chadema bara Tundu Antipas Lissu, katibu mkuu wa chadema John Mnyika na katibu mkuu wa CCM Balozi Dk Emmanuel Nchimbi .
Katika kongomano hilo kulionyesha nini maana ya usawa wa binadamu,umoja wa watu. Hakukuwa na madaraja yaliowagawa waumini katika itikadi za vyama ;nasaba wala kukaa kwa nasabu ya rangi za waumini.
Kwa muktadha huo basi Katibu Mkuu wa TEC Padri Dk Charles Kitima alipoisimama na kuwasimamisha viongozi watatu wa kisiasa nchini akiwemo Lissu ,Dk Nchimbi na Mnyika.Umma ulilipuka na kuliwashangilia viongozi hao kwa sauti za matumaini.
Shangwe na kelele zote za waumini hao , hazikuwa za shangwe kama lile la mashabiki wa simba na yanga ;Small Simba na Malindi au Pamba na Majimaji ; bali zilkuwa sauti za kutuma ujumbe kwa jambo muhimu lifike katika jamii.
Hadi sasa watu kadhaa wamedaiwa kutekwa na kutojulikana mahali walipo. Kila upande umedai upande mmoja unajua mahali waliotekwa mahali waliko na pamoja na kuawawa kwa kiongozi mwanadamizi wa chadema marehemu mtu mmoja Ali Mohammed kibao upande fulani umehusika.
Tuhuma zote hizo zitabaki kama hisia au kupiga ramli kwa mtindo wa bahati nasibu au kucheza tombola.
Waswahili wa kale husema siku zote shaka huwa haishiki mwizi.Kumebiwa na matukio mengi kabla ya matukio ya hivi karibuni ya watu kutekwa na baadhi yao kupigwa risasi na kuawa.
Tiba ya mambo yote hayo haiwezi kuwa majibishano kwenye majukwaa ya kisiasa ,kupitia mitandao ya kijamii, kufanyika kwa mikutano ya hadhara au kuitisha maandamano bila kibali .
Dawa pekee ni watu hususani viongozi kukaa chini ,kuchemsha bongo kwa kushshirikiana na wadau wengine ili kujadiliana, kuukizana maswali na kupeana majibu huku wenye ushahidi wa kina waeleze kinagaubaga.
Kuitisha maandamano hakuwezi kuwa ndio majawabu ya maratizo yote na kupata ufumbuzi wake ;badala yake maandamano yanaweza kuwa chanzo kikuu cha kupoteza kila kitu ikiwemo amani ,utulivu na umoja.
Matokeo ya maandamano tumeyaona kwa nchi kadhaa jirani .Pale waandamanaji wanapopandwa na munkari hadi kufikia kukaidi amri za polisi; ndipo inapozuka piga nikupige ,kamatakatamata na hekaheka kuleta vifo na kuzalisha walemavu.
Viongozi wanapoamua kwa nia moja na nia njema wajifungie ndani ili kujadili hali ya kisiasa na kiusalama,kila jambo litawezekana kupata majibu na tiba ili yasijirudie tena .
Kila kitu chini ya jua kinawezekana kufanyika , kukamilika na kukizuia kitu hicho kisitokee tena na kujirudia .Hivvyo njia pekee muhimu ni wanasiasa kukubali kusimama pamoja kama walivyosimama pamoja kwenye kongamano la ekaristi
Tanzania ndiyo nchi pekee kusini mwa jangwa la sahara yenye sifa ya watu wake kuwa wavumilivu,wasikivu na wenye kupenda mapatano na maelewano.
Ustawi wa aman ya Afrika inategemea sana amani, umoja utulivu wa ndani wa Tanzania, hivyo itakuwa ni kituko kusikia Tanzania ikipoteza amani kwa kushindwa kuelewana wenyewe kwa wenyewe hadi kufikia kuandamana.
Watanzania ikiwa watafikia nukta ya kushindwa kuelewana wao kwa wao,hawatapatanishwa na yeyeote kwakuwa bara zima la Afrika linaitazama Tanzania kama nchi ya mfano kwa ustawi wa Amani ,demokrasia na utawala wa sheria. Tutafika muhimu Uhuru na Kazi.
0 Comments