F Update: Hali ya majeruhi katika ajali iliyoua Wanafunzi Babati. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Update: Hali ya majeruhi katika ajali iliyoua Wanafunzi Babati.



Na John Walter -Babati 

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amewatembelea na kuwajulia hali Wanafunzi wa shule ya Sekondari Endasaki  waliojeruhiwa kwenye ajali ya Coaster na Scania iliyotokea tarehe 31.08.2024 katika Kijiji cha Gajal, Wilayani Babati.

Katika ajali hiyo Watu wanne walifariki dunia, Wanafunzi wakike watatu na dereva wa gari la Coaster aliyekuwa akiwaendesha Wanafunzi wakielekea mkoani Arusha likizo baada ya shule kufungwa.

Sendiga akiongozana  na Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara Maryam Muhaji na Mratibu wa Huduma za Utabibu Mkoa Dkt. Mandala Adam, septemba 01.09.2024 watembelea  majeruhi watatu (3) wote vijana wa kike wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara.

Aidha, Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara Dkt. Catherine Magali alieleza kwamba majeruhi hao watatu waliopo hospitalini hapo wanaendelea na matibabu na afya zao zinaendelea kuimarika.

Jumla ya majeruhi 9 wamepewa rufaa, hospitali ya Kanda Benjamini Mkapa (2), KCMC (7). 

Majeruhi wengine (4) wamehamishiwa hospitali ya Mount Meru kuendelea na huduma na kuwa karibu na ndugu na jamaa. 

Pia majeruhi wengine 15 (wanafunzi 14 na mwalimu mmoja) waliruhusiwa kwenda nyumbani baada ya madaktari kujiridhisha kwamba afya zao zimeimarika.

Jumla ya majeruhi walioletwa katika ajali hiyo na kupokelewa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Manyara walikuwa 31 ambapo kati yao Vijana wa kike ni 26 na wa kiume 5.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga ametoa  pongezi kwa timu ya Afya Mkoa (RHMT) na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kazi kubwa waliyofanya wakati wakitoa huduma kwa majeruhi hao.

Post a Comment

0 Comments