Na John Walter -Manyara
Wanafunzi 48 wa shule mbalimbali za sekondari wilayani Simanjiro mkoani Manyara, wamebainika kupata ujauzito ndani ya kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga, wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo wilayani Simanjiro na kuzungumza na wakuu wa shule za sekondari za mkoa huo katika Mji wa Mirerani.
Mkuu wa Mkoa ameeleza kusikitishwa na hali hiyo, akilaani tabia ya baadhi ya wanafunzi na wazazi kuficha ujauzito kwa kudai kuwa watoto ni watoro.
Amewasisitiza wazazi na walimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo katika malezi ya watoto na kuhakikisha wanaume wanaowadanganya wanafunzi, wakati kuna wanawake wazima wamejaa mitaani, wanachukuliwa hatua kali.
0 Comments