Katika maadhimisho ya wiki ya Huduma kwa Wateja mwaka huu, wakurugenzi wa Airtel Tanzania wameonesha dhamira yao ya kuendelea kutoa huduma kwa wateja kwa kuwahudumia ana kwa ana katika mikoa mbali mbali hapa nchini.
Mkurungezi wa Mawasiliano, Beatrice Singano, Oktoba 8, 2024 aliungana na kitengo cha Huduma kwa wateja na kuongea na wateja kadhaa kupitia simu akiwatakia heri ya siku ya huduma kwa wateja Pamoja na kuwapa taarifa mbalimbali juu ya huduma na bidhaa mbalimbali za Airtel Tanzania.
Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Airtel Money, Andrew Rugamba, akiwa katika ziara ya maduka mbalimbali alizungumza na wateja waliotembelea baadhi ya maduka ya Airtel katika wiki hii. Bw. Rugamba alitumia muda huo kwa kuelezea wateja huduma zinazopatikana katika maduka yote nchini hasa wakati huu wa msimu wa wiki ya huduma kwa wateja. Pamoja na hayo aliwaonyesha wateja mbalimbali simu janja zinazopatikana kwa gharama nafuu na zinaweza kulipiwa kidogo kidogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja, Adriana Lyamba alikuwaduk ala Airtel jijini Arusha, ambapo alitembelewa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mh. Amir Mkalipa na kujadiliana naye kuhusu umuhimu wa huduma bora kwa wateja na jinsi Airtel inavyoendelea kuboresha uzoefu wa wateja wake nchini kote. Kwa pamoja, walipata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wateja ambapo Adriana aliwashukuru kwa kuichagua Airtel.
Nae Mkurungenzi wa Biashara, Joseph Muhere, akiwa Dodoma, alisherehekea pamoja na wateja wa Airtel akitumia kauli mbiu yao ya ‘SABABU NI WEWE’ na kuzungumza nao mambo mbalimbali yanayohusiana na uboreshaji wa huduma za kampuni ya Airtel Tanzania.
Airtel Tanzania inasherehekea wiki ya huduma kwa wateja kwa leongo la kudhihirisha dhamira ya Airtel kuthamini na kuendeleza usikivu kwa wateja. Airtel wanaikamilisha wiki ya huduma kwa wateja inayoadhimishwa duniani kote ikiwa na kauli mbiu ‘Above and Beyond’ ambapo Airtel imeitafsiri kwa kusema ’ Sababu ni Wewe’ ndio maana huduma na bidhaa za Airtel zinampa mteja zaidi.
0 Comments