F Bibi wa miaka 62 afungiwa umeme baada ya kutoa eneo lake bure liwekwe Transformer,TANESCO wasema "Wananchi walikataa lakini bibi huyu alitoa eneo lake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Bibi wa miaka 62 afungiwa umeme baada ya kutoa eneo lake bure liwekwe Transformer,TANESCO wasema "Wananchi walikataa lakini bibi huyu alitoa eneo lake





Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Njombe limefanikiwa kuingiza umeme na kuuwasha bure katika nyumba ya Bibi Esteli Nyalusi mwenye umri wa miaka 62 ambaye ni mkazi wa kata ya Maguvani halmashauri ya mji wa Makambako ikiwa ni kutoa shukrani kwake baada ya kuruhusu bila vikwazo eneo lake kuwekwa transfoma ili umeme uwafikie wananchi wa eneo hilo kwa kuwa watu wengine walikataa huku yeye akiwa hana wazo lolote la kuingiza umeme kwenye nyumba yake.


Akizungumza mara baada ya kuwasha umeme kwenye nyumba hiyo meneja wa TANESCO mkoa wa Njombe Abdulrahman Nyenye amesema wameamua kuhitimisha wiki ya huduma kwa wateje kwa kumpatia bibi huyo umeme kwa kuwa aliweza kutoa eneo lake huku wananchi wengine wakikataa transfoma kuwekwa kwenye maeneo yao.


"Lakini bibi alijitolea kwamba naomba ikae hapa na hakuwa na doto za kuweza kupata umeme lakini na sisi tumeona ni vema kulipa fadhila kwa kumuwashia umeme ambapo tumesuka waya na malipo yote tumeshamlipia"amesema Mhandisi Nyenye

Hanana Mfikwa ni mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Makambako na diwani wa kata hiyo ya Maguvani ameishukuru TANESCO kwa kufikisha umeme kwenye nyumba hiyo ambapo sasa 99.9% kata hiyo imepata umeme huku asilimia moja ikiendelea kushughulikiwa.


"Katika eneo hili pia kulikuwa na changamoto ya uwekaji umeme ambapo zaidi ya transfoma nne ziliungua lakini mamam huyu kwa moyo wake safi akatoa eneo lake na hatimaye tangu mmeweka transfoma moja mpaka iko salama hivyo basi nitoe wito kwa wananchi wengine waone basi na wao ni sehemu ya maendeleo ya taifa hili"amesema Mfikwa

Awali injinia Amina Ng'imba ambaye ni meneja wilaya TANESCO Makambako amesema bibi huyo amesadia watu wa Maguvani kupata huduma ya umeme kwa kuweka transfoma katika eneo lake hivyo nao wameona umuhimu wa kumsaidia.

Kwa upande wake Bibi Esteli Nyalusi ameshukuru shirika la TANESCO pamoja na serikali ya awamu ya sita kwa kumfungia nishati ya umeme



"Hili ni eneo langu na mwenzangu alishakufa kwa hiyo ninyi mliomba ndio maana niliwapatia kwa kweli nashkuru sana kwa wema wenu kwa kuwa sikutegemea kwamba nitapata umeme"amesema Estelia

Licha ya kumfungia umeme lakini pia TANESCO wamefanikiwa kumnunulia jiko la umeme na mahitaji mengine ya nyumbani ikiwemo mchele na mafuta ya kupikia ili kurudisha kwa jamii katika kuadhimisha kilele cha wiki ya huduma kwa wateja.







Post a Comment

0 Comments