F CCM Manyara yawahamasisha Wananchi Kujiandikisha kwenye daftari la Mkaazi. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

CCM Manyara yawahamasisha Wananchi Kujiandikisha kwenye daftari la Mkaazi.


Na John Walter -Babati 
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Manyara Mheshimiwa Peter Toima amewataka Wananchi wote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Daftari la mkaazi litakaloanza kesho Oktoba 11 hadi Oktoba 20 mwaka huu katika vituo vilivyopo kwenye maeneo yao.

Toima ametoa kauli hiyo Leo Oktoba 10,2024 alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake ambapo alisema kuwa, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi wa Serikali za mitaa na kwamba wananchi wanaenda kuchagua viongozi wa Vijiji, vitongoji, mitaa pamoja na wajumbe wa Serikali za Vijiji na mitaa.

Alisema kuwa, uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu ni takwa la Kikatiba na kisheria ambapo inawataka kuchagua viongozi wa Serikali za mitaa kila baada ya miaka mitano hivyo Wananchi wenye sifa wajitokeze.

"Katika uchaguzi huu muhimu nawasisitiza Vijana wasomi mjitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo za uongozi, hii nchi inahitaji wasomi wenye uwezo wa kuamua na kufanya maamuzi yenye tija huko kwenye mitaa, vijiji au vitongoji" alisema Toima 

Amesema Chama hicho kitaendelea kushinda chaguzi mbalimbali kwa kuwa kinayatekekeza yale waliyoayahidi kwa Wananchi wake Katika chaguzi zilizopita.

Mheshimiwa Peter Toima amesema, sifa za wananchi watakaojiandikisha katika Daftari hilo la mkazi ni awe Rai wa Tanzania mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi,awe mkazi wa kijiji au kitongoji au mtaa ambao uchaguzi unafanyika na awe mwenye akili timamu.

Post a Comment

0 Comments