F DC Kaganda atoa wiki moja kukamilika jengo la mama na mtoto Bashnet | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

DC Kaganda atoa wiki moja kukamilika jengo la mama na mtoto Bashnet



Na John Walter -Babati 

Mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Mtatifikolo Kaganda ametoa wiki moja kukamilika kwa jengo la huduma ya mama na mtoto lililopo katika kituo cha afya cha kata ya Bashnet ili kuwasaidia kina mama waweze kupata huduma kwa urahisi na kuepuka kutembea umbali mrefu kwenda kwenye vituo vingine.

Mkuu wa wilaya ametoa agizo hilo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Bashnet ili kujionea maendeleo ya mradi huo wa kituo cha afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya kwenye kata ya Bashnet iliyopo wilayani Babati, na kugundua kuna uzembe mkubwa katika ukamilishaji wa jengo hilo baada ya kupata taarifa kuwa fundi aliyekabidhiwa kujenga kutofika eneo la kazi kwa wakati na kupelekea mradi kuchukua mda mrefu kukamilika.


“Ninawapa wiki moja kufanya kazi, afya za wananchi ni kipaumbele chetu, kama hela ipo na kila kitu kipo sasa nataka nijue nani anakwamisha, kama hadi kina mama wanalalamika mliwaahidi mwezi wa nane lakini hadi leo hamjakamilisha nyie mnajisikiaje?”

Aidha mkuu wa wilaya amesisitjza kuwa hawatofumbia macho jambo lolote linalokwamisha miradi ya maendeleo na lengo kubwa ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora ikiwemo za afya ili kuwa na taifa lenye afya njema hasa huduma ya mama na mtoto kama ilivyo kipaumbele cha Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

“Tutaweka mkazo na msisitizo ili huduma iweze kupatikana ili lile lengo la mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungato wa Tanzania la kuhakikisha kwamba tunakuwa na vifo sifuri vya mama na mtoto, hivyo tutapambana kuhakikisha mnaipata huduma hiyo kwa haraka.” alisema Kaganda

Awali akizungumza na baadhi ya wakina mama waliokwenda  kupata huduma katika kituo hicho  cha afya cha Bashnet wananchi hao wamesema imekuwa kerok ubwa kwao kwani ahadi ya kukamilika kwa jengo la huduma ya mama na mtoto imekuwa ya muda mrefu tangu mwezi wa nane, hivyo wakaiomba serikali iwasaidie kukamilisha jingo hilo ili wakina mama waanze kupata huduma.

Post a Comment

0 Comments