F Itel Tanzania yamwaga misaada Shule ya Msingi Tandale | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Itel Tanzania yamwaga misaada Shule ya Msingi Tandale


KAMPUNI ya Itel Tanzania imekabidhi msaada wa vifaa na bidhaa mbalimbali katika Shule ya Msingi Tandale, wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, ikiwa ni utaratibu wa kampuni hiyo kurejesha pato lake  kwa wananchi.

Akizungumza leo Oktoba 4, 2024 mara baada ya kukabidhi msaada huo, Ofisa Uhusiano wa Itel Tanzania ,Sophia Msafiri, amesema ni utaratibu wa kampuni hiyo kurejesha pato lake kwa jamii hususan shule, vituo vya watoto wenye mahitaji maalumu na kushiriki shughuli za kijamii.

Msaada uliotolewa ni pamoja na Kompyuta tatu, viti kwaajili ya ofisi ya walimu, vitabu vya wanafunzi, madaftari, mabegi, taulo za kike, vifaa vya michezo na zawadi mbalimbali kwa wanafunzi.

“Itel Tanzania leo tumechagua kutoa zawadi katika Shule ya Msingi Tandale, hii ni kawaida yetu  kusaidia shule za msingi na sekondari. Pia tunasaidia  vituo vya yatima na shughuli za kijamii,” amesema Sophia.

Sophia ameongeza kuwa kampuni hiyo itaendelea na utaratibu huo wa kurejesha faida inayopatikana na hii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za serikali katika kuisaidia jamii.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tandale, Andrew John, ameishukuru kampuni ya Itel Tanzania kwa maaada huo na kueleza utasaidia utoaji wa elimu kwa wanafunzi.

Amesema shule hiyo inazaidi ya wanafunzi 2000 na inaongoza kwa kufaulisha wanafunzi  wilayani Kinondoni, hivyo msaada huo utapngeza ufanisi wa ufundishaji kwa watoto.





Post a Comment

0 Comments