F Naibu waziri Sillo awataka wazazi wazungumze na Watoto wao. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Naibu waziri Sillo awataka wazazi wazungumze na Watoto wao.


Na John Walter-Babati 

Naibu waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mheshimiwa Daniel Sillo amewaasa wazazi na walezi kuzungumza na watoto wao kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu maisha yao kwa uwazi bila kuwaficha ili kuwaokoa wasiingie kwenye mambo mabaya yasiyofaa katika jamii.

Sillo ameyazungumza hayo katika mahafali ya kidato cha nne kwenye shule ya sekondari Matufa iliyopo kijiji cha Matufa, kata ya Magugu Wilayani Babati mkoani Manyara, na kusisitiza kuwa wazazi na walezi wameacha majukumu yao ya msingi hali inayopelekea vijana kujiingiza kwenye matendo ya ukatili wa kijinsia na kuhatarisha usalama wa jamii.

“Ninaomba sana wazazi tusikimbie majukumu ya msingi ya kuongea na vijana wetu, tunalaumu watoto wa siku hizi kwakuwa na wao wametokana na wazazi wa siku hizi, unaposikia kijana mdogo wa miaka 25 amembaka bibi kizee, sisi tupo wapi na tunajitengaje na hiyo dhambi? Kwahyo nawomba wazazi zungumzeni na vijana kwa uwazi mkubwa”.

Kwa upande wake diwani wa viti maalumu kata ya Magugu Naomi Richard Sangu amewasihi vijana kutumia nguvu kazi waliyonayo kujiletea maendeleo na kuacha kufanya vitendo vya ukatili na badale yake wasimamie lengo kuu la kujitafutia maisha yao ili wakuze uchumi wao pamoja na wa jamii kwa ujumla.

“Niwaase vijana waache maramoja tabia hii mbaya na wasimame katika lengo la kutafuta maisha ili na wao wapande kiuchumi na masiha yao yaendelee kuwa sawa”.

Shule ya sekondari Matufa ni shule ya serikali na  ilianzishwa tarehe 9 mwezi wa 1 mwaka 2019 na kuanza kupokea wanafunzi tarehe 4 mwezi wa 2 ikiwa na wanafunzi 174 waliosajiliwa na kati yao wavulana walikuwa 87 na wasichana 87 na walimu wa 5, wa kike 1 na wakiume wa 4 na haya ni mahafali ya tatu tangu kuanzishwa kwa shule hiyo iliyojengwa kama sehemu ya kutatua changamoto ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kwenda shule ya sekondari Magugu lakini pia kuwasaidia kuepuka matendo ya kikatili kwenye njia wanazopita.


Post a Comment

0 Comments