Na Heri Shaaban
Shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko wilayani Ilala, wajivunia mafanikio kitaaluma inafanya vizuri kila mwaka katika matokeo yake ya sekta ya Elimu.
Akizungumza katika mahafali ya kumi na tano ya shule ya Sekondari Uhuru Mchanganyiko Mkuu wa shule hiyo Jamaldini Hassan Mohamed, alisema mwaka 2023 matokeo ya kidato cha nne ufaulu ulikuwa asilimia 78 na matokeo ya kidato cha pili ufaulu asilimia 98 hivyo wana imani kubwa wanafunzi wanahohitimu leo watafanya vizuri zaidi.
Mkuu Jamaldini Haassn alisema shule hiyo ilianza rasmi mwaka 2007 ikiwa na wanafunzi 160 na walimu nane wanafunzi wa kwanza walihitimu mwaka 2010 wanafunzi wahaohitinu mwaka huu 2024 jumla 436 ambapo wanafunzi hawa 237 ni Wavulana na wasichana 199 .
"Shule yetu ya Uhuru Mchanganyiko ina mafanikio makubwa kitaaluma na mwaka huu tumejipanga kufaulisha wanafunzi wote kutokana na maandalizi yao kuwa mazuri kwa ushirikiano wa Walimu wangu na wazazi "alisema Mwalimu Jamaldini.
Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Benki ya NMB na Menejiment yake kwa kuiwezesha shule hiyo meza 100 na viti 100 ambapo msaada huo umesaidia sana mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji
Alisema kupitia msaada huo wa thamani za kujifunzia wamezihirisha kwa vitendo kauli mbiu ya Benki ya NMB haimuachi mtu pia imeunga mkono jitihada za Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wa Uhuru Mchanganyiko kuwa mabalozi wazuri huko wanapoenda wakatangaze mazuri ya Shule hiyo na kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi ya mitihani iliyombele yao kujiepusha na makundi yasio faa .
Aliwataka wawe na maadili mema wasiingie katika mmomonyoko wa maadili washirikiane pamoja na wazazi waweze kusonga mbele kielimu kwani Taifa ili liweze kuendelea lazima watu wake waweze kusoma
Meneja wa Benki ya NMB KARIAKOO Wiliam Nkuna alisema changamoto za shule hiyo watazitatua hivi karibu NMB ina shughulikia shughuli za kijamii ikiwemo sekta ya Elimu.
0 Comments