F Sillo awataka Viongozi wa dini kujenga kizazi chenye maadili. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Sillo awataka Viongozi wa dini kujenga kizazi chenye maadili.



Na Mwandishi Wetu, Morogoro 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo ametoa Wito kwa Viongozi wa Dini kuandaa Taifa lenye Maadili na Hofu ya Mungu chini ya Usimamizi wa Makanisa katika kuimarisha Maadili mema miongoni mwa Vijana na Jamii kwa Ujumla

Sillo aliyasema hayo katika hafla ya Maadhimisho ya miaka 150 ya utume ulimwenguni kwa Kanisa la Waadventista Wa Wasabato iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri mkoani Morogoro, Oktoba 25, 2024

Naibu Waziri alilipongeza Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania kwa kazi nzuri wanazofanya zinazochangia Ujenzi wa Taifa ikiwemo nyanja ya elimu, pamoja na afya ambapo Waaumini wa Kanisa hilo huchangia Damu Salama katika Hospitali zetu kila Mwaka 

Katika hatua nyingine Mhe. Sillo aliwataka Viongozi hao wa Dini kufanya huduma ya Utume kwa kuendelea kuilinda amani ya nchi. 'Amani tuliyonayo ilindwe kwa wivu mkubwa sana na ihubiriwe kupitia ninyi Viongozi wa Dini ambao ni wadau wa Amani nchini. Amesema' Sillo

Aidha alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha kuwa Mwaka huu na Mwaka Ujao kutakuwa na  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu hivyo Taasisi za Dini ziwasisitize waamini wao kuhakikisha wanashiriki kwa wingi ili taifa liweze kupata viongozi wazuri na wenye hofu ya mungu.
 


Kwa Upande wake Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Kusini Mwa Tanzania, Dkt. Godwin Lekundayo alisema Kanisa hilo halijajikita tu katika kutoa  huduma za injili pekee bali linatoa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo za elimu pamoja na Afya bila kubagua imani.

Post a Comment

0 Comments