F Ubalozi wa China na Kampuni ya Oryx Gas watoa mitungi 800 ya gesi na majiko yake | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Ubalozi wa China na Kampuni ya Oryx Gas watoa mitungi 800 ya gesi na majiko yake


UBALOZI WA China kwa kushirikiana na Kampuni ya Oryx Gas Tanzania wametoa mitungi 800 ya gesi yakiwa na majiko yake kwa walimu, madereva na wahudumu wa Serikali
pamoja  na Waandishi wa habari wa Mkoa wa Arusha lengo ni kutekeleza sera ya Serikali ya Tanzania pamoja na China katika  kutunza mazingira.

Hafla hiyo imefanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian ,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Benoit Arama ,Mbunge wa Arusha Mjini pamoja na viongozi wa dini

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kugawa mitungi kwa makundi hayo Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian amesema kuwa wanatambua uhusiano mzuri wa kidiplomasia katı ya nchi hizo lakini pia wanafahamu dhamira ya Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan Hassan katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa lengo la kutunza mazingira

Amesema kwamba sera ya China nayo imejikita katika kutunza ukijani, hivyo watashiriki kikamilifu katika kufanikisha malengo hayo.

Amesisitiza nchi ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ikiwemo ya nishati safi ya kupikia.“China itaendelea kusapoti nishati safi ya kupikia na miradi mingine mingi ya maendeleo itakayoendelea Tanzania,” amesema balozi Mingjian.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Oryx Gas Tanzania Ltd Benoit Araman kuanzia Julai 2021, upatikanaji wa suluhisho la kupika imekuwa mada ya umuhimu mkubwa, chini ya uongozi wa Rais  Dk Samia Suluhu Hassan na leo wako pamoja kuunga mkono utekelezaji wa Programu ya Kupika kwa Nishati Safi nchini Tanzania.

Amesema programu ya nishati safi ya kupikia  itachukua miaka 10 kuwezesha upatikanaji wa Nishati Safi kwa ajili ya kupikia kwa angalau asilimia 80  ya Watanzania ifikapo mwaka 2034. Hivyo kuna haja ya kuungana kufanikisha juhudi hizo.

“Ukizungumza kuhusu nishati safi ya kupikia kwa wanafunzi wenu na katika mikutano na wazazi itachangia kwa kiasi kikubwa kueneza kwa nishati safi ya kupikia nchini Tanzania. Ninyi kuwa watumiaji wa Oryx Gas itasaidia idadi ya watu kuona manufaa ya kupika kwa kutumia LPG na kuipitisha zaidi.

“Naushukuru  Ubalozi wa China nchini Tanzania, kwa ushirikiano wao, ambao umeruhusu makabidhiano ya mitungi ya gesi na majiko yake 800. Kwa kushirikiana na Gambo Foundation “Alama Africa” na Oryx Gas Tanzania, nchi ya China inaonyesha nia na dhamira yake ya kuunga mkono utekelezaji wa programu ya Kupika kwa Nishati Safi nchini Tanzania.

Ametumia nafasi hiyo kueleza kwa kina faida za kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo ya  Uboreshaji wa Afya kwani nchini Tanzania, wananchi 33,000 wanakufa kila mwaka kutokana na kuvuta pumzi ya moshi na chembechembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na Oryx LPG kutaondoa changamoto ya Vifo hivyo.

Hata hivyo amesema Kampuni ya Oryx Gas inafanya kazi kwa bidii kila siku kutekeleza maono ya Rais ya kwamba asilimia 80 ya Tanzania ipate nishati safi ifikapo mwaka 2034. Mpango wa leo na Alama Africa Foundation na Ubalozi wa China nchini Tanzania unachangia katika lengo hilo  kubwa kwa kukabidhi mitungi ya gesi na majiko yake 800. Lazima wafanye  zaidi.

Awali akizungumza kuhusu kampeni ya nishati safi ya kupikia na hatua ambazo wanaendelea kuchukua Mbunge wa Arusha Mjini Mrisho Gambo amesema Oryx Gas imekuwa Kampuni ya kwanza kwa Arusha na wamedhamiria kuunga mkono kampeni ya Rais Samia na wamekuwa mstari wa mbele katika kampeni hiyo.

Amesema hata katika utoaji wa mitungi ya gesi 5000 kwa walimu , Oryx Gas walikubali kutoa mitungi na majiko na leo wameendelea kutoa mitungi ya gesi na majiko yake 800 kwa kushirikiana na Ubalozi wa China pamoja na Alama Africa.

“ Tumetoa mitungi na majiko haya ya gesi kutoka kampuni ya Orxy  kwa sababu inapatikana kwa urahisi, sio tunawapa mitungi hapa alafu mkashindwa kuijaza…pia bei ya kuijaza ni nafuu naamini wote mnaweza kumudi,”  amesema Gambo.

Pia amesisitiza anatambua kazi inayofanywa na Rais Samia katika kuhamasisha nishati lakini pia ni jukumu la wadau mbalimbali kuunga mkono kampeni ya Rais Kama ambavyo wanafanya Oryx Gas na Ubalozi wa China.

Kwa upande wake Sheikh wa  Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) Mkoa wa Arusha Sheikh Shaban Juma Abdallah amesema jamii inapaswa kuhakikisha na kusimamia vizuri misitu yetu na jambo ambalo Rais amealinzisha la nishati safi ya kupikia anastahili pongezi kwani ni Jambo lenye kujenga huruma kwa kizazi cha sasa na baadae.

Amesema misitu ikiwa salama ndio salama ya viumbe hai kwa maana ya binadamu na wanyama, hivyo watatumia nafasi zao kuendelea kuhamasisha nishati safi ya kupikia.

Kwa upande wake Mchungaji Julius Talakwa Laiza aliyemwakilisha Baba Askofu wa KKKT Dayosisi Kaskazini Kati Dk.Godson Abel Mollel  , amesema elimu hiyo ya nishati safi wataendelea kuitoa
Kanisani kwa kuanza na watumishi wa Mungu wenyewe kwa kuhimizana katika vyao na waumini wao Kanisani watawahimiza kwamba wakitumia gesi watakuwa wameokoa mazingira.

Amesema kuni na mkaa imeharibu misitu yetu lakini wakitumia gesi watakuwa wanafanya mambo matatu muhimu wanahakikisha misitu iko salama, hewa safi na watawaambia ni Kazi waliyoachiwa na Mwenyezi Mungu na kusisitiza mazingira yalitengenezwa na Mungu, hivyo ni vema wakawndelea kutunza mazingira.

Amesisitiza kuwa kuni na mkaa vinatoa moshi mwingi ambao unaharibu hewa lakini gesi haiharibu hewa.







Post a Comment

0 Comments