F Udongo wa Manyara umeathiriwa na tindikali | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Udongo wa Manyara umeathiriwa na tindikali


Na John Walter -Babati 

Taasisi ya utafiti wa Kilimo nchini TARI imesema udongo wa katika ardhi ya mkoa wa Manyara umeathiriwa na tindikali kwa 55% hali inayoweza kuhatarisha kilimo endelevu.

Akizungumza kwenye maonyesho ya Mbolea Duniani ambayo kitaifa yanafanyika Manyara Dkt. SIBAWAY MWANGO amesema iwapo wakulima hawatazingatia kupata elimu na kufuata kanuni bora za kilimo cha kisasa huwenda wakaendelea kupoteza mazao kwa 55% hadi 70% ikiwa ni pamoja na kupoteza mbolea kwa kutumia bila kujua mbolea gani inafaa kwenye udongo wa mashamba yao. 

Akizindua maonyesho hayo mkuu wa mkoa wa Manyara amesema mkoa huo una hekta laki 9 zinazofaa kwa kilimo hivyo kuwepo kwa umuhimu wataalamu wa kilimo mkoani Manyara kufuatilia taarifa za hali ya udongo na kilimo kutoka Tari. 

 Maonyesho ya mbolea yanafanyika mkoani Manyara kitaifa mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments