F Wahitimu kidato cha nne watakiwa kujiandikisha kwenye daftari la makazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wahitimu kidato cha nne watakiwa kujiandikisha kwenye daftari la makazi


Na John Walter -Karatu 

Vijana wahitimu wa kidato cha nne waliotimiza umri wa miaka 18 wametakiwa kujitokeza kujiandikisha katika daftari la makazi kuanzia Oktoba 11 hadi 20 ili kujiandaa na uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu. 

Wito huo umetolewa na afisa tarafa ya Mbulumbulu Jumanne Maftaa wakati wa mahafali ya kidato cha nne katika shule ya sekondari Kilimamoja iliyopo Karatu mkoani Arusha.  

Maftaa amesema watakaojiandikisha katika daftari hilo la makazi ndiyo watakaoruhusiwa kupiga kura kuwachagua viongozi wa vijiji, mitaa na Vitongoji. 

Aidha Maftaa ametoa wito kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wanaoendelea na masomo kuendelea kuchangia vyakula kwa ajili ya wanafunzi kupata chakula cha mchana wakati wa masomo yao. 

Amesema uhakika wa chakula shuleni umesaidia kupunguza utoro shule na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi katika shule nyingi za tarafa ya Mbulumbulu. 

Kwa upande wake mkuu wa shule hiyo Monica Mboya ameshukuru ushirikiano wa wazazi. Wqlezi na jamii katika uendeshaji wa shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi. 

Amesema katika mahafali hayo jumla ya wanafunzi 79 wamehitimu masomo yao ya kidato cha nne kati ya wanafunzi 154 waliojiunga na shule hiyo mwaka 2020. 

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Meneja wa kampuni ya & BEYOND Mussa Watara ametoa wito kwa wahitimu wa kidato cha nne kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa manufaa ya kutafuta fursa za kujiendeleza badala ya kuitumia kupata taarifa zisizo na maadili. 

Amesisitiza wazazi kuwaongoza vijana wao kupata muongozo wa kutumia ujio wa teknolojia hasa akili mremba badala ya kuwakataza.

Post a Comment

0 Comments