Na John Walter -Dodoma
Serikali imewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko kwa kunawa mikono kila mara kwa maji tiririka na sabuni na kuepuka kugusana.
Hayo yameelezwa na mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa, akieleza kuwa kwa sasa mkoa huo upo kwenye uangalizi maalum kufuatia tishio la ugonjwa wa kipindupindu.
"Suala la ugonjwa wa kipindupindu, si mikoa ya kanda ya kati tumeathirika na bado mlipuko unaendelea, tunaweza kupumzika wiki moja lakini wiki inayofuata ugonjwa ukaibuka tena, kwa sasa hatuna wagonjwa lakini bado tupo kwenye kipindi cha matazamio, kwa hiyo bado tuna mlipuko" alisema
Amesema ugonjwa wa kipindupindu unazuilika kwa kuzingatia usafi, kula vyakula vya moto wakati wote, kuepuka vyakula vilivyolala (Viporo) na kwamba watu wasipochukua tahadhari inaweze kupelekea wagonjwa kuongezeka.
Kuhusu magonjwa mengine ya mlipuko kama Mpox na marburg, amesema hakuna taarifa kutoka wizara ya afya, lakini amesisitiza tahadhari ni muhimu kwa kuwa magonjwa hayo yameripotiwa kwenye nchi jirani ambazo tunamuingiliano nao.
Virusi vya mpox vimeripotiwa kuenea katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mpox, ambayo zamani iliitwa monkey pox, imeenea katika sehemu za magharibi na kati mwa Afrika.
Mnamo 2022, janga la ulimwengu la mpox liliathiri Ulaya, Australia, Marekani na nchi nyingine.
Marburg ni ugonjwa unaosababishwa na wanyamapori.
Mganga mkuu wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa amefungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari wa mikoa ya Dodoma, Singida na Manyara kuhusu mpango wa serikali wa M-mama unaolenga kutoa msaada kwa wakina mama wajawazito kwa kuwapatia usafiri wa dharura bure kwenda kupata huduma kwenye vituo vya afya au hospitali kwa kupiga simu namba 115.
0 Comments