F Wawili wahukumiwa miaka 30 kwa unyang'anyi wa kutumia Silaha. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wawili wahukumiwa miaka 30 kwa unyang'anyi wa kutumia Silaha.


Na John Walter-Singida

Watu wawili ambao ni George Moshi anayejulikana kwa jina maarufu Kobla, (46), na Edward Leonard, (30), wote wakazi wa Mtaa wa Tambukareli Manyoni, Mkoani Singida wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 kila mmoja kwa kosa la wizi wakutumia silaha aina ya panga.

Watuhumiwa hao kwa pamoja walitenda kosa hilo Juni 17, 2024 usiku katika maeneo ya Tambukareli Manyoni ambapo walinyang'anya viti vya kukunja 5  mali ya Kituo cha mafuta kiitwacho Infinity kilichopo katika mji wa Manyoni 

Aidha,  baada ya washitakiwa kutenda kosa hilo, walikamatwa na Jeshi la Polisi na kufikishwa mahakamani Agosti 16, 2024.

Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama mbele ya Mh. George Felician Hakimu Wilaya ya Manyoni.

Post a Comment

0 Comments