F Wilaya ya Babati imejiandaa kwa ajili ya daftari la Wakaazi | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Wilaya ya Babati imejiandaa kwa ajili ya daftari la Wakaazi



Na John Walter -Babati 

Mkuu wa Wilaya ya Babati mkoani Manyara Emmanuela Kaganda amesema wilaya hiyo ipo tayari Kwa ajili ya kuandikisha Wananchi wake wote katika daftari la Wakaazi kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za mitaa kuchagua Viongozi wa vijiji, vitongoji na Mitaa.

Kaganda amesema hatarajii kusikia mtu yeyote au kikundi chochote kinavuruga zoezi hilo linalotarajiwa kuanza Oktoba 11 hadi Oktoba 20,2024.

Kaganda amezungumza hayo Leo Oktoba 10,2024 ofisini kwake wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kuanza kwa zoezi la uandikishaji wa daftari la wakazi na uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 mwaka huu. 

Amesema maandalizi kwa ajili ya  zoezi hilo yapo vizuri na kwamba kila kitu  kipo sawa.

Aidha amesema kwa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kutakuwa na vituo vya kujiandikisha 408 huku Halmashauri ya Mji wa Babati ikiwa na vituo vya kujiandikisha 93.

Pia ameeleza kuwa hata watu walioko gerezani na wagonjwa watafuatwa nyumbani ili wote waweze kushiriki zoezi hilo muhimu.

Kuhusu wanafunzi  wa shule za sekondari na vyuo nao amesema watapewa nafasi wajiandikishe.

Post a Comment

0 Comments