F Zaidi ya trilioni 2.7 kutumika kujenga barabara kupunguza foleni Dar es Salaam | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Zaidi ya trilioni 2.7 kutumika kujenga barabara kupunguza foleni Dar es Salaam


Serikali inafanya mazungumzo na kampuni ya China Overseas Engineering Group Co. Ltd. (COVEC) ambayo imeonesha nia kuwekeza Dola za Marekani bilioni 1 (zaidi ya Shilingi trilioni 2.7) kujenga barabara zenye lengo la kupunguza kero ya foleni jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia wa Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), David Kafulila wakati alipokuwa akitoa taarifa kwa vyombo vya habari.

 Kafulila amesema mwekezaji huyo tayari na amefanya kazi za awali, kama vile upembuzi yakinifu na uchambuzi wa kiuchumi, na sasa inataka kuingia katika Hati ya Makubaliano na Serikali ili iweze kufanya upembuzi yakinifu kamili ya mradi huo.

Ameongeza kuwa Kampuni ya COVEC inataka kutekeleza mradi huo wa kimkakati kwa njia ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), na kudai kuwa tayari Serikali ipo katika hatua mbalimbali za mazungumzo.

Kafulila, amesema kuwa mwekezaji huyo tayari amefanya kazi za awali, kama vile upembuzi yakinifu na uchambuzi wa kiuchumi.

Ameeleza, Kampuni ya COVEC inataka kuingia katika Hati ya Makubaliano (MOU) na Serikali ili iweze kufanya upembuzi yakinifu wa mradi huo.

“Kampuni ya COVEC inataka kujenga barabara 10 za mazunguko kupunguza foleni jijini Dar es Salaam, Barabara hizo za mazunguko ni pamoja na sita za ndani na nne za nje’, amesema Kafulila.

Aidha alisema, utafiti uliofanywa na Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) mwaka 2020 umebaini kuwa foleni inasababisha biashara kupoteza asilimia 20 za faida zao kutokana na foleni za magari kwenye barabara jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments