F CMSA yazindua mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ''mteja atapata faida hadi 13%'' | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

CMSA yazindua mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ''mteja atapata faida hadi 13%''


MAMLAKA Ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA,) imezindua rasmi mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ambao ni mradi wa pamoja wa kampuni ya Sanlam Investments East Africa Limited na M-PESA Limited ikiwa ni hatua muhimu katika maendeleo ya sekta ya fedha hususani masoko ya mitaji katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuzinduliwa kwa jukwaa hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama amesema uzinduzi wa jukwaa hilo utaimarisha na kuongeza kasi ya malengo ya kuwawezesha kifedha wafanyabiashara binafsi katika ukanda wa Afrika na kupitia M-WEKEZA jukwaa la uwekezaji kwa njia ya simu litawawezesha watu binafsi kupata fursa ya uwekezaji kwa urahisi katika maeneo ya mijini na vijijini kwa kutoa huduma za kifedha.

''Kupitia M-Wekeza mteja anaweza kuwekeza Kiwango chochote na kupata faida mpaka 13% endapo atawekeza fedha zake kwa mwaka mzima na unaweza pata taarifa ya kifedha ya uwekezaji wake muda wowote kiganjani mwake'' amesema.

Ameongeza kuwa mpango huo unatoa fursa za uwekezaji kwa wawekezaji wakiwemo wanawake na vijana hali itakayochagiza maendeleo kwa kuhamasisha akiba ya ndani kupitia uwekezaji, kutengeneza fursa za ajira na kujenga uchumi thabiti wa Taifa.

Aidha uzinduzi wa jukwaa hili pia unaendana na mfumo wa tatu wa kitaifa wa ujumuishaji wa kifedha wa 2023/2028 ambao unasisitiza matumizi ya kidigitali katika usambazaji na utoaji huduma za kifedha.”Amesema.

Pia ameipongeza menejimenti ya Sansalam Investment East Africa Limited na M-PESA Limited kwa jitihada za kuunganisha mifumo yao na kupata kibali cha CMSA ambayo imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kisera, udhibiti na utendaji yanayochagizwa na uimara wa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

"Kazi kubwa ya masoko ya mitaji ni kukusanya rasilimali kutoka kwa wawekezaji na kuzielekeza kwenye uwekezaji wenye tija na kuchochea maendeleo katika Serikali, mamlaka za mitaa, taasisi kubwa na ndogo na kampuni mbalimbali ambazo hutoa fedha zinazoelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo,"amesema CPA Mkama.

Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA CPA. Nicodemus Mkama akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mfuko wa uwekezaji wa M-WEKEZA ambao ni mradi wa pamoja wa kampuni ya Sanlam Investments East Africa Limited na M-PESA Limited
 





Post a Comment

0 Comments