Na John Walter -Babati
Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mheshimiwa Paulina Gekul amewataka Wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanarudisha shukrani kwa Chama cha Mapinduzi kwa kukipa kura nyingi za ushindi kesho Jumatano Novemba 27.
Amewaambia Wananchi kuwa hawapaswi kupeleka kura hata moja kwa upinzani kwa kuwa Maendeleo yote yaliyopo kwenye mitaa yao yamefanywa na Chama cha Mapinduzi chini ya mwenyekiti na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan akisaidiwa na madiwani na mbunge.
"Yaani niwambie ukweli kama ni upinzani ni mimi nilikuwa mpinzani haswa lakini kwa kazi kubwa inayofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi,sioni haja ya kuwa kwa vyama hivyo"
Amesema kwa chama cha Mapinduzi iwe jua au unyeshe mvua ushindi ni mapema kwa kuwa Wana kitu cha kuwaeleza Wananchi.
Gekul amewanadi wagombea wa Chama cha Mapinduzi Mtaa wa Nyunguu, Sawe Sigino na Nakwa.
Kwa Upande wake mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Mjini Babati Elizabeth Marley amewataka Wanaccm wajitokeze kwa wingi kupiga kura mapema kisha warejee nyumbani kusubiri matokeo.
Uchaguzi wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji unafanyika kesho Jumatano Novemba 27,2024.
Jimbo la Babati mjini lina jumla ya kata 8, mitaa 35,a vijiji 13 na vitongoji 54.
0 Comments