F Itel yazindua Simu mpya ya A80 kwa ushirikiano na Airtel | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Itel yazindua Simu mpya ya A80 kwa ushirikiano na Airtel


Kampuni ya simu za mkononi Itel imezinduzi simu mpya na ya kisasa, itel A80 kwa ushirikiano na Airtel Tanzania.

Akizungmza wakati wa uzinduzi wa simu hiyo Meneja masoko wa Itel Sphia Almeida amesema Simu hiyo  ya itel A80 inakuja na muundo wa kisasa na sifa bora zinazowafanya watumiaji wake kufurahia matumizi ya kipekee. 

''Itel A80 inajivunia skrini kubwa ya inchi 6.7 yenye punch-hole, betri yenye uwezo wa 5000mAh inayodumu muda mrefu, na kamera ya 13MP yenye ubora wa hali ya juu kwa picha na video.'' amesema Sphia Almeida

Pia, simu ya itel A80 ina nafasi kubwa ya kuhifadhi data ya GB 128 + GB 8, kuhakikisha watumiaji wana uhuru wa kuhifadhi maudhui yao kwa urahisi. Simu hizi zitapatikana katika maduka yetu yote nchi nzima kwa garama nafuu kwa mkopo au kwa kulipa pesa taslimu.

Kupitia ushirikiano huu, wateja wa Airtel watapata ofa maalum itakayowawezesha kufurahia huduma za intaneti kwa gharama nafuu wanapokuwa na itel A80, hivyo kuboresha zaidi matumizi yao hasa kipindi hiki cha msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka.


Kwa upande wake Meneja Mahusiano kutoka Airtel Tanzania Jennifer Mbuya amesema kuwa uzinduzi wa itel A80 unaonyesha ari ya Airtel Tanzania katika kupunguza mgawanyiko wa kidijitali nchini kupitia teknolojia suluhishi kwa bei nafuu.

“Ushirikiano wetu na itel utaongeza matumizi ya simu kwa watumiaji wa Airtel kote nchini kwa kuchanganya vipengele vya kisasa vya Itel na mtandao bora wa Airtel wenye kasi zaidi. Ushirikiano huu unaonyesha jinsi tunavyojitolea katika kurahisisha maisha ya wateja wetu kupitia bidhaa za kibunifu,” alisema (Jennifer Mbuya).

"Tunayo furaha kuzindua itel A80, simu inayounganisha ubunifu, mtindo, na utendaji. Ushirikiano huu na Airtel unaleta thamani ya ziada kwa wateja wetu kwa kuwapatia simu yenye uwezo wa juu na gharama nafuu. Tunaamini kuwa ushirikiano huu utaimarisha zaidi uzoefu wa watumiaji wetu na kuwasaidia kufikia huduma za mtandaoni kwa urahisi."



Post a Comment

0 Comments