F M-mama Mpango rafiki wa kumlinda Mama na Mtoto | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

M-mama Mpango rafiki wa kumlinda Mama na Mtoto



Na John Walter -Dodoma

Wanawake wajawazito na waliojifungua wametakiwa kutumia huduma ya rufaa na usafiri wa dharura kupitia mfumo wa M-Mama inayosimamiwa na serikali.

Huduma ya M-Mama ilizinduliwa na rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt dkt Samia Suluhu Hassan April 2022 kwa ajili ya huduma za dharura kwa wajawazito, waliojifungua, au watoto wachanga wenye umri wa siku 0-28 kwa lengo la kuokoa maisha.

Mpango huo umesaidia kupunguza vifo wakati wa uzazi kwa asilimia 38 na vifo vya watoto wachanga kwa asilimia 40.

Kupata huduma hiyo unapiga simu namba 115 bila malipo kupitia mtandao wowote wa simu.

Kwa mujibu wa Mratibu wa M- Mama Kitaifa Meshack Mollel, kwa kushirikiana na Shirika la Pathfinder wamewaajiri madereva zaidi ya 4000 katika mfumo usio rasmi ili kuwasaidia wakina mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga ambapo mpaka sasa wamefanikiwa kuwasafirisha wajawazito zaidi ya laki moja na kuokoa maisha yao.

Waandishi wa Habari kutoka Redio za Jamii mikoa ya Manyara, Dodoma na Singida wamejengewa uwezo na shirika la Pathfinder ili kutoa elimu kwa jamii inayowazunguka juu ya Mpango huo.

Post a Comment

0 Comments