F Njombe TC wataka wazazi kuona umuhimu wa kupeleka watoto kwenye shule za malezi (Chekechea) | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Njombe TC wataka wazazi kuona umuhimu wa kupeleka watoto kwenye shule za malezi (Chekechea)

 










Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe mkoani Njombe Erasto Mpete ameagiza wamiliki na wasimamizi wa shule za kulea watoto (Day care) kuzingatia miongozo ya uanzishaji wa shule hizo ikiwa ni pamoja na majengo kuto kuwa na wapangaji wengine ili kuimarisha ulinzi wa watoto.

Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wazazi kwenye mahafali ya kwanza katika kituo cha kulea watoto (Chekechea)  Konga Academy iliyopo Nole kata ya Utalingolo mjini humo.

"Nyumba hizi za kulea watoto inatakiwa ziwe mahususi kwa ajili ya kulea watoto wetu kwa hiyo kazi zote zitakazo kuwa zinafanyika hapa (Kwenye vituo) zilenge na zihusiane na shughuli ya kuwalea watoto katika utaratibu na miongozo"

Aidha ametaka serikali za vijiji kutengeneza sheria ndogo ili wazazi wenye watoto wa umri wa miaka miwili na nusu mpaka minne kuhakikisha wanawapeleka watoto chekechea wapate elimu ya awali itakayo waandaa vema kwenda darasa la kwanza. 

"Kuna watu wanabeza kwamba wakidhani hakuna umuhimu wa kumpeleka mtoto chekechea ni makosa makubwa sana,huku wanaandaliwa vema ili wawe na uwezo mzuri wakiwa shule za msingi"amesema Mpete.

Awali katika mahafali ya watoto  wa Konga Academy,katibu wa kituo hicho bwana Viligilio myamba amesema kuwa changamoto ya ukosefu wa madawati na vifaa vya michezo ni changamoto inayowakabili jambo ambalo Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ameahidi kuzishughulikia mapema changamoto  hizo ili kuboresha kituo hicho.

Christina Konga ni mwalimu na pia ni mmiliki wa kituo Cha Konga Academy amesema kuwa hapo awali jamii ilikuwa haiamini kumpeleka shule mtoto mwenye umri wa miaka miwili lakini Sasa wamebadilika kutokana na Uelewa wanaoupata.

Nao baadhi ya wazazi wenye watoto wanaosoma kwenye kituo hiko Cha Konga Academy wamekiri kuwa kimekuwa na msaada katika kuwaandaa watoto kuelekea elimu ya msingi.

Post a Comment

0 Comments