F Samia&Gekul Cup 2024 kuunda timu ya Jimbo na Vijana 40. | Muungwana BLOG
https://c2p.cleverwebserver.com/dashboard/6a0bec4b-79ba-11ef-ad2b-06f0639468d1

Samia&Gekul Cup 2024 kuunda timu ya Jimbo na Vijana 40.



Na John Walter -Babati 

Mashindano ya mpira wa Miguu ya SAMIA&GEKUL CUP 2024 yamefikia tamati novemba 10, 2024, kwa timu za Eagle FC na Bagara FC  kuchukua ubingwa.

Eagle FC kundi la taasisi ilifanikiwa kushinda mabao 6-0 dhidi ya Bajaji FC huku Bagara kwa Upande wa kata ikiifunga magoli 2-0 Sigino katika fainali zilizochezwa Uwanja wa Darajani uliopo kata ya Babati mjini.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mbunge wa Jimbo la Babati mjini Mheshimiwa Paulina Gekul yalilenga kuibua vipaji vya soka ambapo jumla ya Vijana 40 wamepatikana kuunda timu ya Jimbo.


Akizungumza wakati akihitimisha michuano hiyo, Gekul amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuzipa kipaumbele timu za Tanzania zinaposhiriki Mashindano mbalimbali ya kimataifa kwa kutoa hamasa.


“Na mimi niliona dira nzuri na maono ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukuza michezo nchini, nikaona hapa Babati tusibaki nyuma ndio maana tunaendelea Kuboresha Ligi yetu na mwaka huu niliyaita Samia na Gekul Cup kwa kutambua mchango wake katika sekta hii” alisema Gekul.

Pamoja na hayo Gekul amewataka Vijana na wananchi wote kwa ujumla waliojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura, kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura kuchagua Viongozi watakaowaongoza kwenye mitaa yao Novemba 27 mwaka huu.

Mabingwa wa Samia& Gekul Cup 2024, Timu ya Eagle FC wameibuka na Kitita cha Shilingi Milioni Moja, Bagara Shilingi Milioni Moja na washindi wa pili Bajaji na Sigino wakipokea Shilingi laki tano kila moja.



Pia Mbunge huyo wakati Mashindano yanaanza aligawa mipira  kwenye mitaa 35, Vijiji 13 Kata 8 na Taasisi 27 zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Million ishirini  20,000,000 huku Gharama za uendeshaji wa Ligi hiyo zikiwa zaidi ya Million kumi Tsh 10,000,000 hivyo kufanya Jumla ya Gharama zote kufika zaidi ya Shilingi Millioni thelathini na tatu Tsh 33,000,000.

Akitoa salamu za chama Cha Mapinduzi Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Babati Mjini Ndugu Mohammed Chollaje amempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama Cha mpira wa Miguu Wilaya ya Babati (BDFA) Gerald Mtui ameahidi kusimamia kikamilifu Vijana 40 waliopatikana kwa kuwalea.

Post a Comment

0 Comments